Posted By Posted On

Wema Sepetu atua kwenye tuzo Marekani

NA BRIGHITER MASAKI

MREMBO anayefanya poa kwenye tasnia ya filamu nchini, Wema Sepetu, ametajwa kuwa miongoni mwa mastaa wanaowania  tuzo za Hollywood And African Prestigious Awards (HAPAWARDS 2020) nchini Marekani.

Wema, ameingia kwenye tuzo hizo akiwania kipengele cha Mwigizaji Bora wa kike wa Tamthilia za Kiafrika kupitia tamthilia yake, Karma inayoruka kupitia chaneli ya Maisha Magic Bongo, DSTV.

Katika tuzo hizo zinazitarajia kufanyika Oktoba 18, mwaka huu zimemtaja pia Christian Bella kwenye kipengele cha Msanii Huru wa Kiume wa Kimataifa huku Zari The Boss Lady akitarajiwa kuwa mshereheshaji mdogo (Co Host) wa hafla hiyo.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *