Posted By Posted On

Zuchu aandika historia nyingine YouTube

NA MWANDISHI WETU

MTANDAO wa YouTube umetoa orodha ya nyimbo 100 zinazotrendi duniani (Music videos trending worldwide)  ambapo Tanzania, imefanikiwa kuingia kupitia wimbo, Litawachoma ya Zuchu aliyomshirikisha Diamond Platnumz.

Mapema jana video ya Litawachoma ilifanikiwa kushinka namba 83 katika video 100 zinazotazamwa zaidi duniani, rekodi ambayo ni nadra kuwekwa na mpaka sasa wasanii walioweza kufanya hivyo Afrika ni Wizkid, Davido, Burna Boy, Master KG (Jerusalema) na Diamond Platnumz.

“Nimeamka na habari njema video ya wimbo wetu pendwa Litawachoma niliyomshirikisha Diamond uko namba 83 kwenye on trending YouTube ulimwenguni,” alisema Zuchu.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *