Posted By Posted On

MWAMBUSI AAHIDI KUJENGA KIKOSI TISHIO YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Kocha msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amesema anataka kuwaimarisha wachezaji waweze kucheza kwa spidi naeza kwa spidi na kiwango kile kile bila kuchoka ndani ya dakika 90 hadi 120.

Mwambusi alisema hayo baada ya mechi ya kirafiki kati ya timu yake dhidi ya Mwadui FC iliyofanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex na kushinda bao 1-0, juzi usiku.

Kocha huyo alisema mechi za kirafiki wanazocheza zinasaidia kuimarisha viwango vya wachezaji wake, hasa wale ambao hawachezi mara kwa mara, lakini pia kusahihisha makosa yanayojitokeza.

“Wachezaji wote ni wa Yanga, wamesajiliwa na wanatakiwa kucheza, hivyo wale ambao hawachezi ni wajibu wetu kuwaangalia nao, kuimarisha viwango vyao ili waisaidie timu,”alisema Mwambusi.

Aliongeza jambo lingine ni kwamba anataka kuona wachezaji wake wanacheza katika ubora wa juu kwa muda wote wa mchezo na hii ndiyo itawasaidia kupata ushindi bila tabu.

“Ninataka kuona wanakuwa na uwezo wa kucheza dakika zote 90 hadi 120 bila kuchoka, lakini kwa kiwango kile kile na spidi ile ile. Nadhani baada ya wiki tatu hivi vyote tunavyovifanyia kazi vitaanza kuonekana na kutoa matokeo mazuri zaidi,” alisema Mwambusi.

Kuhusu mchezaji raia wa Angola, Carlos Carlinhos, kocha huyo alisema kuwa bado hajapata utimamu wa mwili wa kutosha, hivyo wana kazi ya kumjenga fiziki ili aweze kufanya kile ambacho watamtuma.

“Bado anatakiwa apate fiziki ya kutosha na akishakuwa vizuri tunaweza kupata kile ambacho tunatarajia zaidi kutoka kwake, zaidi ya faulo na kona,” Mwambusi alisema.

Mwambusi anaiongoza Yanga baada ya mabosi wao kumtimua, Zlatko Krmpotic huku Mrundi, Cedric Kaze, akitarajiwa kuwasili nchini wakati wowote kuchukua mikoba ya Mserbia huyo.

,,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *