Posted By Posted On

NUGAZ AWEKA MSISITIZO, HAKUNA HOFU MECHI YA WATANI WA JADI

Msomaji wa Yanganews Blog:Afisa mhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa hawana hofu na mchezo wao dhidi ya Simba wanaamini wakikutana nao lazima watawafunga bila matatizo.

“Kwanza tulikuwa tunawatamani kukutana nao hao Oktoba 18 kwa kuwa ni namba yetu ya bahati, bahati yao tarehe imepelekwa mbele mpaka Novemba 7, ila hiyo tarehe lazima itafika na tutafanya kweli.

“Ukitazama kwa harakaharaka kwa muda huu bado tupo kwenye ubora, hakuna ambacho wametuzidi kuanzia pointi na mechi za kushinda tupo sawa, na namna ambavyo tunakwenda tunazidi kuwa imara mpaka muda tutakaokutana nao muunganiko utakuwa bora zaidi,” amesema Nugaz.

,,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *