Posted By Posted On

Gwambina yaihofia Mtibwa Sugar

NA GLORY MLAY

NAHODHA wa Gwambina, Jacob Masawe, amesema mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar  unatarajiwa kuwa mgumu, lakini wamejipanga kuvuna pointi tatu.

Gwambina wanatarajiwa kucheza na Mtibwa Sugar Alhamisi wiki hii, kwenye Uwanja wa Gwambina, wilayani Misungwi, jijini Mwanza.

Akizungumza na BINGWA kwa simu kutoka Mwanza jana, Masawe alisema kwa sasa  wanaendelea na mazoezi kuhakikisha wanashinda mchezo huo, kwani walianza ligi kwa kusuasua.

“Mtibwa Sugar si timu ya kuibeza hata kidogo, tunajua utakuwa mchezo mgumu, lakini tunaendelea kufanya maandalizi mazuri na wachezaji wote wapo fiti kwa mchezo.

“Hatutakubali kupoteza mechi hiyo tutaingia uwanjani kucheza mpira kusaka ushindi, tunawaheshimu wapinzani wetu, lakini ndani ya dakika 90 kitaeleweka,” alisema Massawe.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *