Posted By Posted On

Kate Kambi aiweka wazi ‘Mkombozi’

PRETORIA, AFRIKA KUSINI

MWIMBAJI anayekuja kwa kasi kwenye gospo kutoka Pretoria, Afrika Kusini, Kate D Kambi, ameendelea kuwaomba wapenzi wa muziki huo kusikiliza na kutafakari ujumbe muhimu uliopo ndani yake.

Akizungumza na Papaso la Burudani jana, Kambi alisema ndani ya wimbo Mkombozi ameimba visa vya kweli ambavyo vipo kwenye vitabu vitukufu vikionyesha jinsi Mungu amekuwa akiwakomboa wanadamu.

 “Wimbo una siku chache kwenye chaneli yangu ya YouTube, nimeweka mashahiri ya wimbo ambayo ni visa vya kweli mfano ni ule wa Daniel kutupwa kwenye shimo lenye simba na simba hawakumla. Hiyo inaonyesha jinsi gani ambavyo Mungu alikuwa mkombozi kwa Daniel.

“Pia nitoe shukurani kwa SSK Production ambao wameshiriki kukamilisha wimbo huu ambao naamini utawabariki wengi na kuwafanya wasiomtegemea Mungu kuanza kumtegemea,” alisema mwimbaji huyo mwenye asili ya  Uvira, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *