Posted By Posted On

Mastaa watatu wapata watoto

NA BEATRICE KAIZA

IMEKUWA wikiendi ya baraka kwa mastaa watatu kutoka kiwanda cha burudani nchini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Rose Ndauka na Queen Darleen kupata watoto mwishoni mwa wiki.

Rose Ndauka  ambaye mapema mwaka huu alifunga ndoa na mumewe, Haffiyy Mkongwa, Ijumaa iliyopita jijini Dar es Salaam walifanikiwa kupata mtoto wao wa kwanza wa kiume waliyempa jina la Haleem.

Rose ambaye Haleem anakuwa mtoto wake wa pili alisema: “Nina watoto wawili, wa kike Naveen na sasa nimepata wa kiume, namshukuru Mungu kwa hilo.”

Pia siku ya Jumamosi jijini Mbeya katika Hospitali ya Meta, mkongwe wa Hip hop nchini, Sugu alifanikiwa kupata mtoto wake wa pili wa kiume kwa mkewe, Happiness  na wamempa jina la Freeman.

Aidha dada wa Diamond Platnumz, Queen Darleen, mwishoni jijini Dar es Salaam yeye na mumewe, Isihaka walipata mtoto wao wa kwanza anayeitwa Balqis akiwa ni mtoto wa pili kwa msanii huyo.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *