Posted By Posted On

Morgan Heritage waanza kusaka vipaji Afrika

NA CHRISTOPHER MSEKENA

KUNDI nyota la muziki nchini Jamaica, Morgan Heritage, limeanza kutekeleza mradi wake wa kusaka vipaji vya muziki barani Afrika kwa kumsaini msanii wa Nigeria, Fayross kwenye lebo yao, CTBC Music Group.

Akizungumza na Papaso la Burudani jana, msemaji wa kundi hilo, Mojo alisema lebo ya CTBC Music Group imeungana na Sony Music katika kusambaza muziki kidijitali ulimwenguni kote hivyo wasanii wa Afrika ikiwamo Tanzania wataanza kunufaika.

“Tutafanya kazi na wasanii wanaochupikia kwenye sekta ya burudani kwa aina zote za muziki. Hii ina maana kuwa wasanii Watanzania watafikiwa na kupata dili kubwa kama hizi.

“Wimbo mpya wa msanii wetu mpya, Fayross tumepanga utoke Novemba 6, mwaka huu na utaweza kununuliwa na watu wote duniani,” alisema Mojo.

Aliongeza kwa kuwataja wasanii kutoka Tanzania kama Foby, Ruby, Wini, Nash Mc, J Zebra na Lau wa John kuwa wanaweza kufikiriwa kusainiwa na lebo hiyo ya Morgan Heritage.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *