Posted By Posted On

Alliance Girls yabakiza mambo matatu

NA DAMIAN MASYENENE, SHINYANGA

KOCHA wa timu ya Alliance Girls, Ezekiel Chobanka, wanaendelea na maandalizi kwa kasi zaidi kuhakikisha wanafanya vyema msimu ujao wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara.

Akizungumza na BINGWA juzi, Chobanka alisema pamoja na kuondokewa na wachezaji wake muhimu, akiwamo Aisha Khamisi, Janeth Matulanga na Enekia Kasonga, amebakiza mambo matatu kukiivisha kikosi chake.

Chobanka alisema anaendelea kufanyia kazi vitu vingi ndani ya kikosi chake, kwani sehemu kubwa anakijengwa upya.

Alisema kwa sasa anatumia muda mwingi kujenga safu bora ya ulinzi, viungo na ushambuliaji ili waweze kufunga mabao na eneo hilo kinamuumiza kichwa.

“Kuna changamoto kwenye ulinzi mawasiliano siyo mazuri, pia viungo hawachangamki kushambulia na wafungaji hawatumii vyema nafasi, kwa hiyo lazima nifanyie kazi kabla ya kuanza mashindano,” alisema kocha huyo.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *