Posted By Posted On

Cavani: Napenda jinsi Pellistri anavyocheza

MANCHESTER, England

STRAIKA mpya wa Manchester United, Edinson Cavani, anaamini Facundo Pellistri, ataonyesha kipaji chake akiwa na timu hiyo.

Pellistri alisajiliwa na Man United, zikiwa zimebaki saa chache tu usajili wa kiangazi kufungwa.

Kinda huyo mwenye umri wa miaka 18, alikuwa anakipiga Penarol ya Uruguay.

“Ni kijana mzuri mwenye kipaji, ana mengi ya kujifunza lakini ana uwezo pia wa kuonyesha mambo adimu akiwa uwanjani, nimemkubali tangu alipocheza mechi yake ya kwanza akiwa na Penarol,” alisema Cavani.

Cavani na Pellistri wote ni wachezaji wa Kimataifa wa Uruguay, ambao wametua Ligi Kuu England kukinukisha.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *