Posted By Posted On

Lakers vidume NBA, yamzawadia Bryant

LOS ANGELES, Marekani

LOS Angeles Lakers imemuenzi nyota wa mpira wa kikapu wa Marekani, marehemu Kobe Bryant, baada ya kubeba ubingwa wa NBA, usiku wa kuamkia jana.

Ubingwa huo Lakers ni kwaajil ya Kobe ambaye aliwahi kuichezea timu hiyo na badaye kustaafu kabla ya kufariki kutokana na ajali ya Helcopter.

Lakers iliibuka kidedea kwa kuifunga Miami Heat jumla ya vikapu 106-93.

Akizungumza baada ya ubingwa huo, LeBron James, alisema ushindi huo unamaanisha kila kitu kwao na kwa Kobe.

“Hii inamaanisha kila kitu kwetu, nilikuja hapa kwaajili ya kitu kimoja, mafanikio na kuifikisha Lakers mahala panapostahili,” alisema James.

LeBron aliibuka mchezaji bora mwenye thamani (MVP), baada ya kufunga jumla ya pointi 28, ribaundi 14 na asisti 10 katika mchezo huo.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *