Posted By Posted On

Mwadui yaipigia Azam tizi kali

ASHA KIGUNDULA NA VICTORIA GODFREY

WACHEZAJI wa timu ya Mwadui wameendelea kufanya mazoezi makali kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam utakaochezwa Alhamisi wiki hii, kwenye Uwanja wa Azam Complex,  jijini  Dar es Salaam.

Akizungumza na BINGWA Dar es Salaam jana,  Kocha wa timu ya Mwadui, Khalid  Adam, alisema malengo yao ni kuibuka na ushindi ugenini.

 Adam alisema mazoezi hayo anatumia kufanya maboresho  kutokana na kasoro zilizojitokeza katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Yanga ili kuwaweka utayari wachezaji wake.

“Kwa sasa hatuchezi mchezo wa kirafiki, tumecheza Ijumaa iiyopita na Yanga na  jana tumefanya mazoezi asubuhi tutafanya mazoezi ya mwisho ili kujiweka tayari  kuvaana na  Azam,” alisema Adam.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *