Posted By Posted On

NiiteBoshenafunguka anavyotengeneza pesa kwa kuchora tattoo:Awatamani,Neymar,Diamond, Konde Boy

KARIBU msomaji wa Jiachie na Staa Wako, safu  inayokupa nafasi ya kuwauliza maswali watu maarufu katika tasnia ya burudani. Leo tupo na Bryson Peter maarufu kama Niite Boshen, msanii wa michoro ya mwilini maarufu kama tattoo anayoifanya kwa mastaa na watu wa kawaida.

SWALI:  Fadhiri Mataruma wa Tabora anauliza : “Ulianza lini uchora tattoo?

Niite Boshen: Uchoraji ni kitu ambacho kipo kwenye damu, tangu utoto wangu lakini maisha yalivyozidi kukua na kubadilika nikajikuta nimeanzisha biashara ya uchoraji wa ‘tattoo’ na hiyo ni baada ya kutoka kuongeza elimu ya uchoraji huko Nairobi nchini Kenya ila nje ya uchoraji elimu yangu ni diploma ya masuala ya masoko.

SWALI:  Hilary Jumanne wa Kigoma anauliza: “Kuna sanaa nyingi, kwanini uliamua kuwa mchora tattoo?”

Niite Boshen: Ni sababu napenda na huwa nachora michoro yote ila ni baada ya kuangalia wapi naweza kupata wateja wengi ili niweze kupata kipato nikagundua tattoo zinapendwa na wengi hivyo naweza kujtengeneza pesa.

SWALI: Ally Musa a.k.a Docho wa Masasi Mbaju anauliza: “Baada ya kucheza filamu ya Giza la Mchana, kuna filamu nyingine utacheza?”

Niite Boshen: Mpango upo ila inategemea na hiyo dili ya kucheza filamu imekuja kipindi gani na nitanufaika vipi.

SWALI: Hamidu Thomas wa Mdambi anauliza msanii gani amewahi kukulipa malipo makubwa katika kumchora tattoo na ilikuwa tattoo gani?

Niite Boshen: Mastaa wengi nimewachora tattoo ila Rich Mavoko ndio msanii niliyefanya naye kazi na akanilipa vizuri tu, ilikuwa tattoo ya kichwa cha simba ambayo inaonekana kwenye mkono wake.

SWALI: Monica Johnson wa Mwenge, Dar es Salaam anauliza: “Unakabilia vipi na changamoto na mitego ya watoto wa kike wanaohitaji uwachore tatoo kwenye maeneo nyeti ya miili yao?”

Niite Boshen: Naheshimu familia yangu na watu wanaonizunguka, najua namna ya kukabiliana nazo. Kama unavyojua nimemuoa msanii wa Bongo Fleva, Haitham. Hii naheshimu kazi yangu, hata wateja wangu pia, kwangu imekuwa kawaida kwasababu nishafanya kazi nyingi sana.

SWALI: Kally Makuru kutoka Temeke anauliza: “Mke wako ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, Haitham, je ana sapoti kazi yako kwa kiwango gani?”

Niite Boshen: Namshukuru Mungu mke wangu ananiamini sana pia ana thamini kazi yangu na hiyo ni sapoti tosha.

SWALI: Halifa Juma wa Kilwa Masoko anauliza: ‘Mchoraji gani mwingine wa tattoo hapa Tanzania una mhofia?”

Niite Boshen: Binafsi naamini kila mtu ana sanaa yake kwahiyo kila mtu anafanya kazi kwa muda na nafasi yake, sidhani kama kuna kuhofiana.

SWALI: Suleiman Rajabu wa Tandika anauliza : “Mtu akitaka kuchora tattoo ana kupata vipi?

Niite Boshen: Anaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii natumia jina la Niite Boshen au anaweza kuja ofisini kwangu moja kwa moja nipo pale maeneo ya Kijitonyama Police Mabatini hapa na Dar es Salaam.

SWALI: Msanii gani unatamani kumchora tattoo?

Niite Boshen: Nje natamani kumchora mchezaji wa mpira Neymar na hapa Tanzania natamani sana kuwachora wasanii wawili wa muziki ambao ni Diamond Platnumz na Harmonize wamekuwa wakipenda sana sanaa hii ya tattoo.

Wiki ijayo tutakuwa na Gigy Money au Tonton Fwamba, mwanamuziki kutoka Kentucky nchini Marekani, tuma swali lako kwake kupitia namba hapo juu, tuma meseji tu.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *