Posted By Posted On

CHAMA ACHOTA MILIONI 460 YANGA

NA WINFRIDA MTOI KLABU ya Yanga imemtengea kitita cha fedha shilingi milioni 460 kiungo wa Simba, Clatous Chama, endapo atakubali kujiunga na kikosi hicho mwishoni mwa msimu akimaliza mkataba na Wanamsimbazi hao. Chama aliyejiunga na Simba Julai 2018 akitokea Lusaka Dynamos ya nchini kwao Zambia, anatarajia kumaliza mkataba wake na Wanamsimbazi hao, Julai mwakani. Kiungo
The post CHAMA ACHOTA MILIONI 460 YANGA appeared first on Gazeti la Dimba.,

NA WINFRIDA MTOI

KLABU ya Yanga imemtengea kitita cha fedha shilingi milioni 460 kiungo wa Simba, Clatous Chama, endapo atakubali kujiunga na kikosi hicho mwishoni mwa msimu akimaliza mkataba na Wanamsimbazi hao.

Chama aliyejiunga na Simba Julai 2018 akitokea Lusaka Dynamos ya nchini kwao Zambia, anatarajia kumaliza mkataba wake na Wanamsimbazi hao, Julai mwakani.

Kiungo huyo amekuwa akihusishwa na Yanga tangu msimu uliopita kabla ya kuongeza mkataba mwingine na Wanasimba wamekuwa katika mgogoro na Wanayanga baada ya mchezaji huyo kutajwa Jangwani.

Kutokana na Chama kuwa kipenzi cha Wekundu wa Msimbazi hao, akikubalika na mashabiki kwa sababu ya kiwango chake, hakuna anayetaka kusikia habari za nyota huyo kuondoka hasa kwenda kwa watani zao.

Pamoja na yote, Yanga imeendelea kukomaa ikisubiria mchezaji huyo amalize mkataba ili waanze kumshawishi, huku ikitenga kabisa dau la kumpa.

Habari ambazo DIMBA Jumatano imezipata ni kwamba Yanga imefikia hatua ya kutenga fedha za usajili wa mchezaji huyo baada ya kubaini haonyeshi dalili za kuongeza mkataba Msimbazi huku ikidaiwa amewaambia viongozi wa Simba kuwa amepata timu Afrika Kusini.

Kutokana na sababu hiyo, Wanajangwani hao wanadaiwa kuwa fedha waliyotenga inaweza isifikiwe na timu anayotaka kwenda mchezaji huyo, hivyo itakuwa rahisi kumnyakua.

“Viongozi wa usajili walichofanya ni kuandaa fedha tu za kumpa mchezaji huyo, lakini hakuna mazungumzo yoyote yanayoendelea kwa sababu yule mchezaji ana mkataba na itakua kosa kisheria, wanasubiri mwakani,” kilisema chanzo hicho.

Inadaiwa kuwa kitendo cha Yanga kutenga dau hilo, ni kejeli wanazopata wakiambiwa hawana uwezo wa kumsajili Chama au mchezaji yoyote wa kiwango chake.

Hata hivyo, hivi karibuni Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Haji Manara, alivyotembelea kampuni ya New Habari (2006) Ltd, wachapishaji wa magazeti ya DIMBA, BINGWA, MTANZANIA na RAI, alisisitiza mchezaji huyo hawezi kucheza Yanga.

Manara alisema Yanga haina uwezo wa kumsajili Chama, wala mchezaji anayeendana na nyota huyo kwasasa.

Kocha mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, aliwahi kuweka wazi kuwa kiwango anachokionesha mchezaji huyo kikiendelea, wanaweza kumkosa msimu ujao.

The post CHAMA ACHOTA MILIONI 460 YANGA appeared first on Gazeti la Dimba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *