Posted By Posted On

DAKTARI YANGA ATHIBITISHA, BALAMA KULIANZISHA HIVI KARIBUNI

Msonaji wa Yanganews Blog:Kiungo fundi, Balama Mapinduzi anayekipiga ndani ya Yanga baada ya kuwa nje ya Uwanja kwa muda mrefu taratibu ameanza kurejea kwenye ubora wake.

Daktari wa timu ya Yanga ameweka wazi kuwa muda mfupi kuanzia sasa kiungo huyo ambaye msimu uliopita aliingia kwenye orodha ya wachezaji waliofunga mabao bora atarejea kazini.

Bao lake moja kati ya matatu aliyofunga ndani ya Yanga kwenye Ligi Kuu Bara kabla ya kupata jerahaย  katika kifunda cha mguu msimu uliopita Juni, mwaka huu alimtungua mlinda mlango namba moja wa Simba Aishi Manula akiwa nje ya 18 Januari 4, kwenye sare ya kufungana mabao 2-2.

Shecky Ngazija, daktari wa Yanga amesema kuwa hali ya kiungo huyo inaendelea vizuri na tayari ameshaanza kuufanyia mazoezi mguu wake jambo linalotoa matumaini ya kurejea kwake ndani ya uwanja hivi karibuni.

โ€œBalama Mapinduzi anaendelea vizuri tangu kaumia kiwiko cha mguu wa kushoto miezi mitatu iliyopita, wiki iliyopita tulimfanyia vipimo vya mwisho ambavyo vinaonyesha kwamba yupo tayari kuanza kufanya mazoezi mepesi.

โ€œJambo la kufurahisha ni kwamba Balama ameshaanza kufanya mazoezi mepesi chini ya uangalizi wa madaktari na ikiwa mambo yatakwenda sawa basi tunatarajia kumuona akicheza mechi zijazo,โ€ amesema.

,,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *