Posted By Posted On

Kaze kutua na mifumo mitatu

NA WINFRIDA MTOI KOCHA mpya wa Yanga, Mrundi Cedric Kaze, anatarajiwa kutua kesho kuanza kazi ya kukinoa kikosi hicho kujiandaa na mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara. Kaze anatua Jangwani kuchukua nafasi ya Mseribia, Zlatko Krmpotic, aliyefukuzwa baada ya uongozi kutoridhishwa na mwenendo wa kikosi hicho. Kocha huyo raia wa Burundi, anawasili akiwa tayari ameisoma
The post Kaze kutua na mifumo mitatu appeared first on Gazeti la Dimba.,

NA WINFRIDA MTOI

KOCHA mpya wa Yanga, Mrundi Cedric Kaze, anatarajiwa kutua kesho kuanza kazi ya kukinoa kikosi hicho kujiandaa na mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kaze anatua Jangwani kuchukua nafasi ya Mseribia, Zlatko Krmpotic, aliyefukuzwa baada ya uongozi kutoridhishwa na mwenendo wa kikosi hicho.

Kocha huyo raia wa Burundi, anawasili akiwa tayari ameisoma timu hiyo na ndiye aliyeshauri kusajiliwa kwa kiungo wa Vital’O, Said Ntibazonkiza.

Ntibazonkiza alisajiliwa na Wanajangwani hao baada ya kumaliza mechi ya kirafiki juzi kati ya Burundi na Taifa Stars na ndiye aliyefunga bao la pekee la timu yake iliyoshinda 1-0 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Inadaiwa kuwa usajili huo ni kutokana na mifumo mitatu anayokuja nayo Kaze katika kuhakikisha anakisuka upya kikosi cha Yanga.

The post Kaze kutua na mifumo mitatu appeared first on Gazeti la Dimba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *