Posted By Posted On

SIMBA WAIUNDIA MKAKATI MZITO TANZANIA PRISONS

NA WINFRIDA MTOI SIMBA imeamua kuja na mkakati kabambe wa kuhakikisha wanamaliza jeuri ya Tanzania Prisons ambayo imekuwa ikiwasumbua kwenye kwenye mechi zinazochezwa Nyanda ya Juu Kusini. Msimu uliopita, Simba iliambulia pointi mbili katika michezo yote miwili na haikufanikiwa kufunga bao hata moja baada ya kutoka suluhu. Wanamsimbazi hao wanatarajia kukutana na Prisons Oktoba 22
The post SIMBA WAIUNDIA MKAKATI MZITO TANZANIA PRISONS appeared first on Gazeti la Dimba.,

NA WINFRIDA MTOI

SIMBA imeamua kuja na mkakati kabambe wa kuhakikisha wanamaliza jeuri ya Tanzania Prisons ambayo imekuwa ikiwasumbua kwenye kwenye mechi zinazochezwa Nyanda ya Juu Kusini.

Msimu uliopita, Simba iliambulia pointi mbili katika michezo yote miwili na haikufanikiwa kufunga bao hata moja baada ya kutoka suluhu.

Wanamsimbazi hao wanatarajia kukutana na Prisons Oktoba 22 mwaka huu kwenye Uwanja wa Mandela, mjini Sumbawanga.

Simba itacheza kwa mara ya pili katika uwanja huo, mara ya mwisho ulikutana na Namungo, Agosti mwaka huu kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) na kutwaa ubingwa.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wamekuwa wakijifua vikali tangu wiki iliyopita, huku programu ikibadilika na kuwepo mazoezi ya gym.

Mashabiki wa timu hiyo, wameanza mipango maalumu ya kuhakikisha wanakwenda Sumbawanga kukisapoti kikosi chao kama walivyofanya mechi ya ASFC.

Lengo la mashabiki hao kwenda kwa wingi, ni kutaka kuvunja mwiko kwa kuifunga timu hiyo, inayowasumbua mara nyingi, huku wajivunia kikosi chao kuwa ni tofauti na misimu mingine.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, meneja wa timu hiyo, Patrick Rweyemamu, alisema programu za mwalimu zinaendelea kama kawaida kujiandaa na mechi hiyo hadi siku watakayoondoka.

“Benchi la ufundi linaendelea na mazoezi ya kujiandaa na mechi zetu zote za Ligi Kuu Bara, mojawapo ni hiyo ya Prisons, tutaweka wazi siku tunayoondoka kwenda Sumbawanga,” alisema.

Kabla ya kukutana na Prisons, Wanamsimbazi hao walikuwa wamepanga kucheza mechi mbili za kirafiki, lakini ya jana imeahirishwa na mchezo mwingine wanatarajia kukutana na Mlandege ya Zanzibar, Uwanja wa Azam Complex.

The post SIMBA WAIUNDIA MKAKATI MZITO TANZANIA PRISONS appeared first on Gazeti la Dimba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *