Posted By Posted On

AFC kuilipua Geita Gold

NA VICTORIA GODFREY

KOCHA timu ya Arusha FC, Atuga Manyundo, amesema hatafanya makosa kwani malengo yaliyopo ni kuibuka na ushindi dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Daraja la  Kwanza  Tanzania Bara utakaochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Nyankumbu.

Katika mchezo uliopita wa ligi hiyo, Arusha FC  ilifungwa mabao 2-1 dhidi  ya Pamba uliochezwa kwenye Uwanja wa Nyamagana, jijini Mwanza.

Akizungumza na BINGWA jana kwa simu kutoka Mwanza, Manyundo alisema wamejipanga kupambana na wapinzani wao kuhakikisha wanapata pointi tatu.

Manyundo  alisema wachezaji wake wanaendelea na mazoezi  ya mwisho kuelekea mchezo huo.

 “Mchezo wa kwanza na Pamba tulipoteza na umepita sasa macho, akili na nguvu zetu tumeweka na kuangalia  mchezo ulio mbele yetu na Geita Gold,” alisema Manyundo.

Kocha  huyo alisema  wachezaji wote wana hali nzuri  na wanajipanga kuhakikisha wanapata matokeo bora na kutimiza malengo ya kupanda daraja msimu ujao.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *