Posted By Posted On

Bosi La Liga anaamini Messi atabaki

 Hispania hata baada ya BARCELONA, Hispania RAIS wa La Liga, Javier Tebas, anaimani nahodha wa Barcelona, Lionel Messi, ataendelea kucheza sokalake Juni 2021 mkataba wake utakapomalizika. Messi mwenye umri wa miaka 33 alitaka kuondoka Barca Agosti mwaka huu baada ya kuchoshwa na namna klabu hiyo ilivyokuwa inaendeshwa kabla ya kubadili maamuzi pale vigogo hao wa Catalunya walipotaka euro milioni 700 ili kumuachia. “Messi? Ninaimani ataendelea kubaki La Liga,” alisema Tebas. La Liga ilimpoteza Cristiano Ronaldo miaka miwili iliyopita baada ya straika huyo Mreno kuondoka Real Madrid na kusaini Juventus mwaka 2017, Neymar akaondoka Barcelona kujiunga na PSG. “Cristiano Ronaldo aliondoka miaka miwili iliyopita lakini hatukujua athari yake kwa mtazamo wa kiuchumi,” alisema Tebas.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *