Posted By Posted On

Chidi Beenz awafokea Diamond, Kiba, Harmonize

 NA BRIGHITER MASAKI

STAA wa Hip hop nchini, Rashid Makwilo a.k.a Chidi Beenz, amewataka wasanii wakubwa, Diamond Platnumz, Ali Kiba na Harmonize kuwashika mkono wasanii wenzao.

Akizungumza na Papaso la Burudani hivi karibuni, Chidi Beenz alisema muziki hauwezi kushikiliwa na wasanii watatu pekee bali riziki inatakiwa igawanywe kwa wasanii wote.

“Sasa hivi popote unapoenda wasanii wanaopata shoo ni watatu tu, Harmonize, Diamond na Ali Kiba. Hawa wanatakiwa kuwashika mkono wasanii wenzao na sio kila siku wanafanya wao tu,” alisema Chidi anayetamba na wimbo Blood.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *