Posted By Posted On

KAZE AFURAHIA KUTUA YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Kocha mpya wa Yanga Mrundi Cedric Kaze amesema anajivunia kujiunga na vigogo hao nchini na kuahidi kufanya makubwa.

Kaze huenda akatua wakati wowote kuanzia leo kujiunga na timu hiyo ya Jangwani, Kariakoo akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Kocha Mserbia, Zlatko Krmpotic aliyetupiwa virago kutokana na klabu hiyo kutoridhishwa na mfumo wake katika timu.

Kaze aliandika ujumbe kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter jana, akielezea namna anavyojivunia kuwa Kocha wa mabingwa hao mara 27 wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara.

“Ninajivunia kuwa  kocha  wa timu yenye historia kubwa, mashabiki wa aina yake, moja ya timu bora Afrika…. Pamoja tutafanya makubwa,”aliweka ujumbe huo akiwa ameambatanisha na picha ya tukio la wiki ya Mwananchi la mwaka huu, ambalo Yanga walijaza Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Yanga inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kwa pointi 13 baada ya kucheza michezo mitano na kati ya hiyo kushinda minne na kupata sare moja nyuma ya watani zao Simba wanaoshika nafasi ya pili kwa pointi sawa na vinara Azam FC yenye pointi 15.

Mtihani wa kwanza wa Kaze Yanga huenda utakuwa ni ule dhidi ya Polisi Tanzania utakaopigwa Oktoba 22 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

,,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *