Posted By Posted On

Kiba awapa mchongo Bongo Muvi

NA JEREMIA ERNEST

KATIKA kuadhimisha miaka 21 ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, staa wa muziki nchini, Ali Kiba, amemwomba Rais  Dk. John Magufuli,  fungu la kuwawezesha wasanii wa filamu kutengeneza makala ya maisha ya mwasisi huyo.

Akizungumza mbele ya maelfu ya wakazi wa Dar es Salaam waliojitokeza jana kwenye kampeni za urais wa Chama Cha Mapinduzi, Kiba alisema filamu na makala itakayochezwa na wasanii wa Tanzania itakuwa kumbukumbu nzuri kwa vizazi na vizazi.

“Nikuombe Rais wetu kwa kuwa leo (jana) ni kumbukumbu ya Baba wa Taifa, tunaomba iandaliwe bajeti itakayoweza kutengeneza filamu na makala ya Mwalimu Nyerere kupitia wasanii wa filamu ili hata wadogo zetu na watoto wetu wajue aliyoyafanya Mwalimu Nyerere kwenye nchi yetu,” alisema Kiba baada ya kutumbuiza.

Naye Rais Magufuli, alionyesha kulipokea ombi hilo kwa kutingisha kichwa na kupiga makofi.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *