Posted By Posted On

Meja Mingange aisifia Mbeya City

NA ZAINAB IDDY

BAADA ya timu ya Mbeya City kuanza vibaya Ligi Kuu Tanzania  Bara, Kocha wa kikosi cha Lipuli, Meja Mstaafu wa Jeshi, Abdul Mingange,

amesema kikosi hicho kinachofundishwa na Amri Said  kina wachezaji wazuri,  lakini kinakosa utulivu katika maamuzi uwanjani.

Kauli ya Meja Mingange imekuja baada ya kumalizika kwa  mchezo wa kirafiki  dhidi Mbeya City  ulimalizika kwa  wapiga nyundo hao kuibuka na ushindi wa mabao 4-3.

Akizungumza na BINGWA jana, Meja Mingange alisema kwa jinsi wachezaji wa Mbeya City walivyocheza  wanaonekana ni wazuri, lakini wanakwama kupata matokeo bora kutokana na kukosa utulivu wanapokuwa langoni kwa mpinzani.

“Sijawahi kuwaona Mbeya City kabla msimu huu na nimekuwa nikisikia matokeo wanayoyapata hadi kufikia kuwa wa mwisho katika msimamo wa ligi, nilivyowaona,  swali la kwanza kunijia ni hawa wanaocheza ligi au wengine.

“Nilijiuliza hivyo kwa sababu niliona timu nzuri  na inapambana uwanjani, lakini hawapati matokeo kwa sababu sio watulivu kwenye kumalizia hasa wanapokuwa ndani ya eneo la hatari ni vizuri,  Amri azungumze na vijana wake wanahitaji kuwa na nidhamu kubwa ya  mchezo uwanjani,” alisema Meja Mingange.

Mbeya City  kwa sasa wanashika mkia katika msimamo wa ligi hiyo kutokana na pointi moja, baada ya kucheza michezo mitano, ikifungwa minne na sare moja huku Azam wakiongoza kwa pointi 15.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *