Posted By Posted On

Murray amkubali Nadal

LONDON, England

REKODI ya Rafael Nadal ya kubeba mataji 13 ya French Open, haitavunjwa na mchezaji yoyote wa tenisi kwa mujibu Andy Murray. Nadal, mwenye umri wa miaka 34, aliibuka kidedea baada ya kumshinda mkali mwenzake, Novak Djokovic, wikiendi iliyopita. “Sidhani kama rekodi yake itavunjwa, kamwe haitajirudia tena,” alisema Murray. Mkongwe wa mchezo wa tenisi, Bjorn Borg, anashika nafasi ya pili, akiwa amebeba mataji sita ya French Open, kuanzia mwaka 1974 na 1981.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *