Posted By Posted On

Namungo, Biashara zaua, Ihefu FC hoi

NA GLORY MLAY

TIMU ya Namungo  imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa,mkoani Lindi, ukiwa ni mwendelezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katika mchezo huo, Kagera Sugar walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 19 kupitia kwa Yusuph Mhilu, kabla ya Hashim Manyanya kuisawazishia Namungo dakika ya 22 na  baadaye Bigirimana Blaise kuongeza la pili dakika ya 65.

Mchezo mwingine wa ligi hiyo, Ruvu Shooting iliondoka na pointi tatu baada ya kuifunga JKT Tanzania bao 1-0 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Bao la washindi hao lilifungwa na David Richard dakika ya 46 ambalo lilidumu hadi mwisho wa mchezo huo.

Biashara United  walipata ushindi  wa bao  1-0 dhidi ya Ihefu kwenye Uwanja wa Karume, jijini Musoma, mkoani Mara.

Katika mchezo mwingine,  Timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC), imeshindwa kupata pointi tatu badaa ya kutoka suluhu na Coastal Union, kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *