Posted By Posted On

Neymar ampiku Ronaldo, sasa amtafuta Pele

RIO, Brazil

FOWADI wa Brazil, Neymar alikuwa moto wa kuotea mbali baada ya kufunga mabao matatu ‘hat trick’ kwenye ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Peru katika mchezo wa kutafuta tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia mwaka 2022.

Mabao hayo matatu yanamfanya Neymar anayeitumikia PSG kumpita mkongwe Ronaldo de Lima ambaye alikuwa akikamata nafasi ya pili katika orodha ya wafungaji wa muda wote wa Brazil. Neymar amefikisha mabao 64, mawili zaidi ya Ronaldo huku akiwa nyuma kwa mabao 13 kufika kwa gwiji wa soka Brazil, Pele ambaye ni kinara wa muda wote akiwa na mabao 77.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *