Posted By Posted On

Ronaldo kumkosa Messi kisa Corona

TURIN, ITALIA. SUPASTAA wa Juventus, Cristiano Ronaldo yupo hatarini kukosa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Barcelona baadaye mwezi huu kutokana na janga la corona. Shirikisho la soka la Ureno lilithibitisha juzi kuwa mshindi huyo mara tano wa Ballon d’Or alipimwa na kukutwa ma maambikizi ya corona na hivyo atalazimika kujitenga kwa wiki mbili. Kwenye hatua ya makundi, Juventus imepangwa na Barcelona huku mechi yao ya kwanza ikitarajia kupigwa Oktoba 28, ambapo Ronaldo angekutana na mpinzani wake wa siku zote, Lionel Messi. Mechi ambazo hazina mjadala kwamba Ronaldo atazikosa ni zile za Crotone, Dynamo Kiev na Hellas Verona zitakazofanyika akiwa karantini, huku kukiwa na wasiwasi mkubwa kama atacheza dhidi ya Barca. Ronaldo amefunga mabao matatu katika mechi mbili alizocheza Serie A msimu huu.,Read More

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *