Posted By Posted On

Tory Lanez apigwa mkwara mzito

LOS ANGELES, MAREKANI

MAHAKAMA mjini Los Angeles, Marekani, imempiga mkwara mzito rapa, Tory Lanez, asimkaribie mrembo Megan Thee Stallion kwenye kipindi chote  cha kesi yao inapoendelea.

Tory Lanez ambaye anakabiliwa na kesi ya kumshambulia Megan kwa kumpiga risasi ya mguu, Septemba mwaka huu, Jumanne wiki hii alipandishwa kizimbani kusikiliza shtaka lake kwa mara ya kwanza.

Mbali na kuwekewa zuio hilo, Tary Lanez amewekwa mahabusu kusubiri tarehe nyingine ya kusomwa kwa kesi yake huku akitarajiwa kutoa dhamana ya shilingi milioni 440 ili asubiri kesi yake akiwa nje.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *