Ulimboka ataka pointi tatu nyumbani
NAVICTORIA GODFREY
KOCHA timu ya Pamba, Ulimboka Mwakingwe, amesema wamejipanga kuibuka na ushindi dhidi ya Singida United katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara, utakaochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Nyamagana, jijini Mwanza.
Pamba walianza ligi hiyo kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Arusha FC katika mchezo uliopita uliochezwa kwenye uwanja huo.
Akizungumza na BINGWA kwa simu kutoka mkoani Mwanza juzi, Mwakingwe alisema wataende;ea kupata ushindi dhidi ya Arusha FC.
Mwakingwe alisema malengo yao ni kuhakikisha wanarejea Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao, baada ya kushuka daraja kutokana na kufanya vibaya.
“Pamoja na ushindi tulikuwa tumepanga tufunge mabao zaidi ya hayo tuliyopata , lakini tunamshukuru Mungu vijana wamefanya yale niliyowaelekeza na sasa tunahitaji kutimiza malengo yetu ya kuutumia uwanja wa nyumbani kupata matokeo,” alisema Mwakingwe.
Amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kuwasapoti kwa moyo ili waweze kufanya vizuri na baadaye kutimiza malengo yao.
,
Comments (0)