Posted By Posted On

KAZE ATINGA NCHINI, APANIA MAKUBWA YANGA

CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga amewasili Kwenye ardhi ya Bongo usiku wa kuamkia leo kwa ajili ya kuanza majukumu mapya ndani ya timu hiyo.

Kaze ambaye alikuwa nchini Canada amekuja kuchukua mikoba ya Zlatko Krmpotic ambaye alifutwa kazi Oktoba 3 na uongozi wa Yanga.

Wakati akiondoka alikuwa amekiongoza kikosi cha Yanga Kwenye mechi tano za Ligi Kuu Bara  ambapo alishinda nne na kupata sare moja ya kufungana bao 1-1 na Tanzania Prisons,  Uwanja wa Mkapa.

Kaze amesema kuwa anafurahi kuja Bongo kujiunga na timu ya Yanga kwa kuwa anatambua ni timu kubwa yenye malengo makubwa na mashabiki wengi.

“Nimefurahi kuja kujiunga na Yanga ambayo ni timu kubwa na inajulikana ukanda wa Afrika Mashariki na kati hivyo uwepo wangu hapa utakuwa na faida pia.

“Ninajua kuhusu malengo ya timu na kile ambacho wanahitaji hivyo ninaweza kuwaambia kwamba wasiwe  na mashaka katika hilo,” amesema

 

,,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *