Posted By Posted On

Guardiola amtetea Aguero

MANCHESTER, England

KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola, amemtetea, Sergio Aguero, kwa kitendo chake cha kumzonga mwamuzi msaidizi, Sian Massey-Ellis.

Tukio hilo limetokea katika mechi ya Ligi Kuu England, Manchester City ilipomenyana na Arsenal.

Aguero alimzonga mshika kibendera huyo ambaye ni mwanamke akipinga maamuzi aliyotoa huku akimgusa mabegani.

“Jamani embu tuachaneni na mambo hayo, Aguero ni kijana mzuri tu, tafuteni sababu nyingine lakini kwa hili hapana,” alisema Aguero.

Katika mtanange huo Man City iliifunga Arsenal bao 1-0.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *