JKT Tanzania Vs Tanzania Prisons Tangu mwaka 2018, Prisons imefungwa mara moja tu na JKT Tanzania na ilikuwa mwaka 2018 kwenye …

JKT Tanzania Vs Tanzania Prisons

Tangu mwaka 2018, Prisons imefungwa mara moja tu na JKT Tanzania na ilikuwa mwaka 2018 kwenye mchezo wa ligi kuu bara, Leo wanakutana watoto wa jeshi wote wawili pale Jamhuri Dodoma, Ubaya ni kwamba JKT haijawahi kushinda hata mchezo mmoja kwenye uwanja wake wa nyumbani tangu kuanza kwa msimu huu

Mtibwa Vs Namungo

Tofauti ya Namungo na Mtibwa ni sare tangu kuanza kwa ligi Namungo haijawahi kupata sare hata moja ni kufungwa mara 3 na wameshinda mara mbili upande wa Mtibwa wao, michezo waliocheza kwenye uwanja wao wa Nyumbani hawajawahi kushinda zaidi ya kutoa sare dhidi ya Ruvu Shooting tu, Uzuri wa Namungo mchezo wake wa mwisho nje ya nyumbani wameshinda

Coastal Union Vs Biashara United
.
Iko hivi michezo miwili ya mwisho ya Biashara wameshinda wakiwa nyumbani na hii ndio inaweza kuwa kawaida yao kwenye uwanja wa nyumbani tangu kuanza kwa ligi lakini wakitoka nje wanafungwa tena vizuri tu, Coastal Union bado haijaleta muunganiko mzuri tangu ligi imeaza wameshinda mara moja tu na kutoka sare mara moja uzuri ni kwamba michezo yote waliocheza nyumbani ndo wamevuna pointi hizo 4.

Polisi Tanzania Vs Gwambina

Hawa watoto wa kota sio watu wa mchezo kwenye michezo sita hii wamefungwa mara moja tu tena dhidi ya Azam, Gwambina ya Mwanza bado kama inakuja inakataa hivi kwenye michezo sita ameshinda miwili tu na kutoka sare mara moja akifungwa mara tatu na haijawahi kushinda nje ya uwanja wake wa nyumbani.
.
#M9Updates

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *