Posted By Posted On

MSOLLA APELEKA ONYO KWA MASHABIKI YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Mwenyekiti wa klabu ya Yanga ,Dkt Mshindo Msolla akiongea na waandishi wa habari kuhusu ujio wa kocha mpya , Cedric Kaze, amesema sasa ni wakati wa wanachama, Mashabiki na wapenzi wa klabu hiyo kongwe zaidi nchini kumpa Ushirikiano mkubwa kocha na klabu kwa ujumla ili malengo yao yatimie .

Msolla amekwenda mbali kwa kusema , huu sio wakati wa kumpa pressure kocha ya kumpangia kikosi au kuanza kumsema mitandaoni kwa kutompanga mchezaji fulani .

“ ni wakati sahihi wa kumuacha kocha aitengeneze timu na kuipanga atakavyo yeye kwakuwa ndio anaekuwa nao kambini na kufahamu nani acheze na nani asicheze kulingana na mbinu zake , mifumo na sababu nyingine muhimu kwake “ alisema Msolla .

Msolla amewataka wanachama wa klabu hiyo kutoa ushirikiano pekee wa kuhudhuria kwa wingi mechi za timu hiyo pia kuinadi vyema popote walipo ili kurudisha makali ya klabu hiyo ambayo yamedumu katika hii nchi kwa zaidi ya miaka 80.

“ tujifunze uvumilivu na kuwaacha watu wafanye kazi zao kulingana na taaluma zao . Huyu ni mwalimu mzuri na binafsi nina imani nae kubwa kutupa kile ambacho tunakitarajia kwa masilahi mapana ya klabu yetu “ – Msolla.

Kaze ametua Yanga akitokea nchini Canada alipokuwa akifundisha soka la vijana na tayari ameanza kazi rasmi ya kuiandaa timu hiyo kwa michezo ya ligi kuu Tanzania bara akifungua ukurasa dhidi ya Police Tanzania tarehe 22 October, 2020 uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

,,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *