Posted By Posted On

Mugalu: Bocco, Kagere poa tu!

NA ASHA KIGUNDULA

MSHAMBULIAJI wa timu ya Simba, raia wa DR Congo, Chriss Mugalu, amesema uwapo wa  wapachika mabao wenzake, Meddie Kagere na John Bocco, utampa nafasi ya kuwania ufungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu na anafurahi akipangwa na mojawapo.

aliyejiunga na Simba katika msimu huu wa Ligi Kuu Bara, tayari ameifungia timu yake mabao matatu, baada ya kucheza michezo sita.

Akizungumza na BINGWA jijini Dar es Salaam juzi, baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Mlandege  uliochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Mugalu alisema timu hiyo ina wachezaji wazuri wenye uwezo mkubwa wa kuipa ushindi.

Mugalu alisema kuwa kiu yake ni kufunga idadi kubwa ya mabao na kuweka rekodi ya wafungaji bora wa misimu iliyopita.

“Nikipangwa na nahodha wetu Bocco na Kagere nitafika huko na kupita, najua uwezo wao ni mkubwa na hata wengine wanafanya vizuri, lakini hawa wanaweza kunifanya nipambane zaidi,” alisema Mugalu.

Mugalu ambaye katika mchezo huo  dhidi ya Mlandege alifunga mabao mawili,  alisema, amefurahi kuona washambuliaji Ligi Kuu Bara ,kila moja anapambana ili kuwa kinara wa mabao na kuweka rekodi zilizopita  kama ilivyo kwake.

 “Mimi najua kuna wachezaji wenzetu ni majeruhi, nawaombea wapone na kurudi uwanjani, wote tukicheza pamoja nina imani kubwa ya kufika mbali na kuchukua mataji yote tunayopambania,”alisema Mugalu.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *