Posted By Posted On

Mwadui wakomalia mabao ya mipira iliyokufa

NA ZAINAB IDDY

KOCHA wa timu ya Mwadui, Khalid Adam,ameweka wazi kuanzia sasa atawaandaa baadhi ya nyota wake kwa ajili ya kupiga mipira iliyokufa kwa usahihi ili waweze kuvuna mabao mengi msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kauli  ya Adam imekuja baada ya kuona wakosa nafasi nyingi  ambazo zingewawezesha kupata mabao katika michezo yao ya ligi hiyo  kwa wachezaji wake kushindwa kupiga  kwa ufanisi mipira iliyokufa.

“Katika michezo sita tuliocheza tumepata nafasi ya kupiga mipira iliyokufa  saba, lakini yote hiyo hakuna hata mmoja uliotupa mabao, binafsi sijapendezwa na jambo hili.

“Baada ya kutambua hilo nilianza kulifanyia kazi mara baada ya mechi yetu na Azam na kuwatengeneza wachezaji maalumu wa kutupa mabao kupitia mipira hiyo,”

Adam alisema kesho (leo) wana mchezo dhidi ya Mbeya City utampa picha namna gani aliowapa kazi wanatekeleza kwa ufanisi pale itakapotokea nafasi ya kupiga mipira ya namna hiyo.

Mwadui wamecheza michezo sita katika ligi hiyo hadi sasa na kuvuna alama sita wakiwa wameshinda michezo miwili na kupoteza minne wakiwa nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi msimu huu.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *