Posted By Posted On

Real Madrid, Barca zachezea vichapo

MADRID, Hispania TIMU ya Cadiz ambayo ilipanda ligi msimu huu, imeichapa kipigo cha kushtua, Real Madrid cha bao 1-0 wikiendi iliopita. Cadiz ilipata ushindi huo kwa mara ya kwanza ikiwa ni muda mrefu tangu miaka 30 iliyopita. Straika wa timu hiyo, Anthony Lozano, ndiye aliyefunga bao la pekee katika mchezo huo. Madrid walionyesha kiwango kibovu na katika mchezo huo walipiga mashuti mawili tu dhidi ya Cadiz. Katika hali ya kushangaza Barcelona nayo ilipokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Getafe. Bao pekee katika mchezo huo ilifungwa na straika, Jaime Mata, kipindi cha pili kwa mkwaju wa penalti. Mata alifunga penalti hiyo dakika ya 56 kufuatia, Frenkie de Jong, kumchezea vibaya, Djene Dakonam. Lionel Messi aligongesha mchuma kipindi cha kwanza huku Antoine Griezmann akipaisha shuti lake. Huku ikiwa zimebaki dakika tano mpira kumalizika, Juan Hernandez, naye aligongesha mchuma kwa timu ya Getafe.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *