Posted By Posted On

Robert Lewandowski

MUNICH, Ujerumani

STRAIKA wa Bayern Munich, Robert Lewandowski, amefikisha mabao 102 katika mechi 100 alizocheza na miamba hiyo ya Bundesliga.

Lewandowski alivunja rekodi hiyo akifunga mabao mawili katika mechi ambayo Bayern Munich walishinda 4-1 dhidi ya Arminia Bielefeld. Kwa ushindi huo, Bayern inalingana pointi na Borussia Dortmund, wote zikiwa na pointi tisa kwenye msimamo wa ligi. Dortmund wao walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Hoffenheim, bao ambalo liliwekwa kimiani na Marco Reus.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *