Posted By Posted On

Rooney ahofia kupata corona

LONDON, England

NAHODHA wa Derby County,Wayne Rooney, amelazimika kupima virus vya corona huku akihofia huenda amepata maambukizi.

Rooney alijawa na hofu hiyo baada ya rafiki yake ambaye alipata maambukizi ya virusi vya corona, kumtembelea nyumbani kwake.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, Rooney alichukizwa na kitendo cha rafiki yake huyo, Josh Bardsley, kumtembelea kwa lengo la kumpa saa ya thamani.

Rooney alisema Josh alihatarisha afya za familia yake pamoja na wachezaji wenzake, baada ya kuvunja sheria ya kujikinga na ugonjwa huo hatari.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *