SVEN AJA NA USHINDI KIMBUNGA KOCHA wa Simba, Sven Vanderbroeck, amesema licha kupata upinzani mkali kutoka kwa Yanga na Azam …

SVEN AJA NA USHINDI KIMBUNGA
KOCHA wa Simba, Sven Vanderbroeck, amesema licha kupata upinzani mkali kutoka kwa Yanga na Azam katika vita ya ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, ana amini kikosi chake kitaendelea kupata ushindi wa kimbunga utakaobeba kutetea lao kwa mara ya nne mfululizo
Kwa sasa Simba wanashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo kutokana na pointi 13, sawa na Yanga, lakini wakitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa huku Azam wakiwa kileleni kwa pointi 18.
Kutokana na matokeo hayo, Vanderbroeck alisema jijini Dar es Salaam juzi, wakati Simba ikicheza na Mlandege ya Zanzibar katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, kuwa wanajipanga vizuri kuhakikisha anapata ushindi wa mabao mengi Ligi Kuu Bara.
Katika mchezo huo, Simba ilishinda mabao 3-1 ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons utakaochezwa Alhamisi wiki hii kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, mjini Sumbawanga, mkoani Rukwa.
Vanderbroeck alisema kuwa, ana matumaini makubwa kikosi chake kitaendelea kupata ushindi sambamba na idadi kubwa ya mabao ambayo yatakuja kuwa na faida mwishoni mwa msimu huu.
Kocha huyo alisema kuwa, kutokana na ubora wa safu yake ya ushambuliaji, inayoongozwa na Middie Kagaere, John Bocco na Chris Muguli ana uhakika wa kufunga bao zaidi ya moja katika kila mchezo wa ligi hiyo.
#BimgwaOnline

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *