Posted By Posted On

VAN DIJK KUFANYIWA UPASUAJI WA GOTI UNAOWEZA KUMUWEKA NJE MUDA MREFU

BEKI wa Liverpool, Virgil van Dijk atakwenda kufanyiwa upasuaji wa goti la kulia baada ya kuumia kufuatia kugongana na kipa wa Everton, Jordan Pickford katika derby Merseyside iliyoisha kwa sare ya 2-2 Uwanja wa Goodison Park Ligi Kuu ya England Jumamosi.
Japo Liverpool haijasema Van Dijk atakuwa nje kwa muda gani, lakini kwa asili ya maumivu yake – beki huyo wa kimataifa wa Uholanzi atakosekana kwa muda mrefu.
Van Dijk alicheza kwa dakika sita kabla ya kugongana na Pickford na nafasi yake kuchukuliwa na Joe Gomez kufuatia kutibiwa kwa dakika tano bila mafanikio na sasa Mwanasoka huyo Bora wa Mwaka England 2018-19 atakosekana kwenye LIgi Kuu kwa mara ya kwanza tangu September 2018.

Hapa ndipo Virgil van Dijk alipoumizwa na kipa Jordan Pickford (chini) kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Jumamosi Uwanja wa Goodison Park PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *