Posted By Posted On

AZAM FC YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI LIGI KUU TANZANIA BARA YAICHAPA IHEFU SC 2-0 SOKOINE

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
AZAM FC imeendeleza rekodi yake nzuri ya kushinda kila mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara hadi sasa msimu huu – baada ya leo pia kuwachapa wenyeji, Ihefu SC 2-0 Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Ushindi huo uliotokana na mabao ya viungo washambuliaji Ayoub Lyanga dakika ya 55 na Iddi Suleiman ‘Nado’ dakika ya 83 wote wakimalizia kazi nzuri za Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo unaifanya Azam FC ifikishe pointi 21 baada ya kucheza mechi saba.
Azam FC sasa wanawazidi mabingwa watetezi, Simba SC na mabingwa wa kihistoria, Yanga SC pointi nane, ingawa vigogo hao wana mechi mbili mkononi.

Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Ruvu Shooting imetoa sare ya 1-1 na KMC Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, Mwadui FC imeichapa Mbeya City 2-1 Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga na Kagera Sugar imelazimishwa sare ya 0-0 na Dodoma Jiji FC Uwanja wa Kaitaba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *