Posted By Posted On

Klabu ya Mbeya City leo tarehe 20/10/2020 imesitisha rasmi mkataba wa kazi na Mwl. Amry Said Juma kama kocha mkuu wa klabu hiyo….

Klabu ya Mbeya City leo tarehe 20/10/2020 imesitisha rasmi mkataba wa kazi na Mwl. Amry Said Juma kama kocha mkuu wa klabu hiyo.

Maamuzi haya yamefikiwa baina ya pande mbili baada ya majadiliano kutokana na mwenendo usioridhisha wa timu yetu inayoshiriki katika ligi kuu inayoendelea.

Mwl. Amry Said alijiunga na Mbeya City Disemba mwaka jana ikiwa katika mzunguko wa pili wa michezo ya ligi Kuu 2019/2020.

Katika kipindi hiki cha mpito timu itakuwa chini ya Mwl. Msaidizi Mathias Wandiba. Klabu inachukua nafasi hii kumshukuru Mwl. Amry Said kwa kazi yake nzuri na ya kukumbukwa aliyoifanya katika timu yetu katika muda wote aliyohudumu kama kocha mkuu.

E.E.Kimbe
AFISA MTENDAJI MKUU
MBEYA CITY FC

#sokaplaceupdates

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *