Posted By Posted On

Rais wa klabu ya Zamalek ya nchini Misri Mortada Mansour (68) ametangaza kuwa ametoa bonasi ya pauni za Misri 50,000 (Tsh milion…

Rais wa klabu ya Zamalek ya nchini Misri Mortada Mansour (68) ametangaza kuwa ametoa bonasi ya pauni za Misri 50,000 (Tsh milioni 7.3) kwa kila mchezaji kama bonasi ya ushindi wa mchezo wa nusu fainali ya kwanza dhidi ya Raja Casablanca wa bao 1-0 uliopigwa Juzi Jumapili nchini Morocco.

Bonasi hizo amepata kila mchezaji wa Zamalek aliyeshiriki na kwa ambaye hajashiriki katika mechi hiyo, na pia Mansour ameahidi kutoa tena bonasi hiyo kama watashinda mchezo wa marudiano utakaopigwa Misri Jumamosi hii Oktoba 24.

Pia Mansour ameahidi kuwa endapo watafanikiwa kuchukua Ubingwa, wachezaji hao watapata bonasi ambayo hawajawahi kuiona awali.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *