Posted By Posted On

CARLINHOS KUREJEA DIMBANI HIVI KARIBUNI

Msomaji wa Yanganews Blog:Meneja wa kikosi cha Yanga, Hafidh Saleh, amesema kiungo wao, Carlos Carlinhos, hajaumia sana kwa kuwa alipata mshtuko kwenye mazoezi hivyo mashabiki wasiwe na mashaka.

Kocha wa kikosi hicho, Cedric Kaze, amethibitisha kuwa nyota huyo ataukosa mchezo wa kesho dhidi ya Polisi Tanzania baada ya kuumia juzi katika mazoezi ya timu hiyo Kigamboni jijini hapa.

Muangola huyo ambaye amekuwa na kiwango kizuri kwasasa baada ya kufunga bao moja na kupiga pasi za mwisho mbili katika michezo mitatu iliyopita ya Yanga.

Akizungumza na chanzo chetu, Salehe aliwataka mashabiki kutokuwa na presha kwani nyota huyo hajapata majeraha makubwa yatamkayomfanya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu.

“Kweli Carlos alipata majeraha lakini si makubwa sana kwasasa hivyo mashabiki wasiwe na mashaka katika hili atarejea kwenye ubora wake.

“Kwasasa kikosi kinaendelea na maandalizi kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Polisi Tanzania, mashabiki wajitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu yao,” alisema Salehe.

Mbali na Carlinhos, nyota mwingine atakayeukosa mchezo huo ni kiungo, Abdulaziz Makame.

,,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *