Posted By Posted On

Follow @mawele_jr Yes!, VPL inaendelea kushika kasi, zipo timu zilizocheza mzunguko wa 7 na nyengine zikiwa na mechi za vipolo …

Follow @mawele_jr

Yes!, VPL inaendelea kushika kasi, zipo timu zilizocheza mzunguko wa 7 na nyengine zikiwa na mechi za vipolo mikononi mwao.

Tuachane na hayo, tumtazame golikipa wa Dodoma Jiji FC anaeitwa Aron Kalambo.
Huyu ni mlinda mlango ambae Dodoma Jiji FC walimsajili kutoka kwa Wana KomaKumwanya “Mbeya City FC”.

Aron Kalambo amewahi pia kuitumikia Tanzania Prisons misimu michache iliyopita.

Mpaka sasa ndani ya VPL amefanikiwa kucheza mechi 7 na kati ya hizo amevuna clean sheet 6.
Hiki ni kiwango bora sana kwa golikipa anaeichezea klabu kama Dodoma Jiji FC.

Hii ni aina ya klabu ambayo inaruhusu mashambulizi ya mara kwa mara hivyo basi uimara mkubwa sana wa Aron Kalambo umeifanya klabu hiyo kutoruhusu goli lolote katika mechi 6 kati ya 7.

Yupo David Kissu Mapigano, anafanya vizuri sana kwa sasa lakini kwa upande wangu Aron Kalambo naona anafanya vizuri zaidi.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *