Posted By Posted On

Kocha wa klabu ya Yanga Mrundi Cedric Kaze amesema washambuliaji timu yake Michael Sarpong na Yacouba Sogne hawafungi kwasababu …

Kocha wa klabu ya Yanga Mrundi Cedric Kaze amesema washambuliaji timu yake Michael Sarpong na Yacouba Sogne hawafungi kwasababu viungo hawatimizi majukumu yao ipasavyo

“Tangu nikiwa nchini Canada nilikuwa nalijua tatizo lililopo katika timu ambalo ni safu ya ushambuliaji kushindwa kufunga mabao, tatizo ambalo ninaamini nitalifanyia kazi kwa haraka ili kuhakikisha wanafunga.

“Washambuliaji akina Sarpong na Yacouba, wameonekana kushindwa kufunga mabao kutokana na viungo wao kushindwa kutimiza majukumu yao vizuri, ikiwemo kuwapa mipira mizuri ya kufunga mabao.

“Hivyo nimeanza kuiboresha safu hiyo ya ushambuliaji kwa kuhakikisha natengeneza muunganiko mzuri wa viungo na washambuliaji ambao kabla ya kuja kwangu haukuwepo”.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *