Posted By Posted On

SIMBA YAIKOKIA BUNDUKI PRISONS

NA MOHAMED KASSARA INYESHE mvua liwake jua, Simba imeapa kuondoka na pointi tatu muhimu kesho dhidi ya maafande wa Tanzania Prisons ili kukoleza mbio za kutetea taji lao la ubingwa wa Ligi Kuu Bara. Prisons watakuwa wenyeji wa mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga ambapo jeshi la Simba litakuwa chini ya Chris
The post SIMBA YAIKOKIA BUNDUKI PRISONS appeared first on Gazeti la Dimba.,

NA MOHAMED KASSARA

INYESHE mvua liwake jua, Simba imeapa kuondoka na pointi tatu muhimu kesho dhidi ya maafande wa Tanzania Prisons ili kukoleza mbio za kutetea taji lao la ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Prisons watakuwa wenyeji wa mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga ambapo jeshi la Simba litakuwa chini ya Chris Mugalu na Larry Bwalya waliopewa kazi maalumu ya kuwamaliza maafande hao.

Msafara wa kikosi cha wachezaji 22 na benchi la ufundi linaloongozwa na Sven Vandenbroeck umetua mjini humo kwa lengo la kusaka pointi tatu dhidi ya Wajela jela hao.

Baada ya kukosekana kwa Meddie Kagere na John Bocco, safu ya ushambuliaji ya Simba inatarajiwa kuongozwa na Mugalu ambaye amekuwa moto wa kuotea mbali tangu atue nchini.

Mpachika mabao huyo raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo (DRC) amefunga mabao saba katika michezo sita aliyocheza Simba.

Mugalu amefunga mabao matatu kwenye michezo mitatu ya Ligi Kuu Bara na mengine manne katika michezo ya kirafiki na kumfanya kuweka rekodi ya kipekee.

Mshambuliaji huyo ataongoza jahazi baada ya Bocco kubaki Dar es Salaam akiendelea na mazoezi mepesi, huku Kagere naye akikosekana kutokana na kupata majeraha kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania.

Bwalya naye atabeba majukumu ya nduguye, Clatous Chama, ambaye yupo nchini Zambia kukamilisha taratibu za kupata hati mpya ya kusafiria.

Kiungo huyo amekuwa akitoa burudani ya nguvu kwa mashabiki wa timu hiyo kutokana na uwezo mkubwa wa kuchezea mpira, atakuwa na jukumu la kuhakikisha anatengeneza za kutosha za mabao katika mchezo huo.

Kukosekana kwa Chama kutamfanya Sven kumpa Bwalya kazi ya kuratibu mipango yote ya mashambulizi ya Simba (playmaker) ndani ya eneo la hatari la wapinzani wao.

Mbali na Chama, Kagere na Bocco, wengine wanaokosekana katika mchezo huo ni pamoja na Pascal Wawa aliye nchini kwao Ivory Coast akifuatilia hati ya kusafiria, Gerson Fraga anayeuguza majeraha.

Simba itaikabili Prisons ikitoka kuvuna ushindi mnono ugenini wa mabao 4-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wao wa mwisho uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Prisons itakutana na Simba ikitoka kulazimisha sare ya bao 1-1 na JKT Tanzania katika mchezo wao uliochezwa juzi Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Kikosi hicho kinachonolewa na kocha Salum Mayanga kimevuna pointi sita katika michezo yake sita waliyoshuka dimbani hadi sasa, ikishinda mchezo mmoja, sare tatu na kupoteza miwili.

Hata hivyo, rekodi za msimu uliopita baina ya timu hizo mbili zinaonyesha haitakuwa kazi rahisi kwa Simba kuondoka na pointi tatu.

Licha ya kutangazia ubingwa kwa Prisons msimu uliopita, Wekundu hao wa Msimbazi hawakufanikiwa kuifunga timu hiyo katika michezo miwili waliyokutana.

Mbali na Simba kushindwa kuvuna pointi mbele ya Prisons, pia haikuthubutu hata kutikisa nyavu za Wajela jela hao ndani ya dakika hizo 180.

The post SIMBA YAIKOKIA BUNDUKI PRISONS appeared first on Gazeti la Dimba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *