Posted By Posted On

ALICHOSEMA KAZE BAADA MECHI YA LIGI KUU DHIDI POLISI TANZANIA

Msomaji wa Yanganews Blog:Baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania kocha wa klabu ya Yanga, Cedric Kaze amesema kupata matokeo ndani ya siku tano sio kitu rahisi.

Mchezo huo ulikuwa wa kwanza kwa kocha huyo ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara toka alipojiunga na timu hiyo wiki iliyopita.

Kaze amesema kuwa ameona mabadiliko kwenye kikosi chake ndani ya muda mfupi licha ya mwanzo wa mchezo wachezaji wake walikuwa wanapoteza pasi kirahisi.

β€œKupata matokeo ndani ya siku tano sio kitu chepesi, polisi ni timu nzuri na haijafungwa kirahisi kwenye ligi, kitu nilichopenda ni wachezaji wangu kucheza mwanza mpaka mwisho,” alisema kocha huyo.

Bao pekee la Yanga kwenye mchezo wa leo lilifungwa na kiungo wake Tunombe Mukoko dakika ya 70.

Baada ya matokeo hayo Yanga wanakwenda mpaka nafasi ya pili kwenye msimamo kwa kufikisha pointi 15, huku Simba ikishuka nafasi ya tatu baada ya kupoteza dhidi ya Tanzania Prisons.

,,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *