Amri adai chake Mbeya City
NA ASHA KIGUNDULA
ALIYEKUWA kocha wa timu ya Mbeya City, Amri Said, amesema hana anachosubiri zaidi ya kupewa haki zake baada ya uongozi wa klabu hiyo kuvunja mkataba wake.
Juzi uongozi wa Mbeya City ulitangaza kumtimua kocha huyo kutokana na mwenendo wa matokeo mabaya ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Akizungumza na BINGWA jana, Amri alisema viongozi wake ndio waliomuondoa hivyo ana haki ya kupata anachostahili kwa kuwa aliwafanyia kazi.
Amri alisema juzi alikutana na viongozi wa klabu hiyo na kutaka maelezo kutokana na mwenendo wa timu yao na nini anatakiwa kifanyike ili timu iweze kufanya vizuri.
Kocha huyo alisema anashangaa kusikia mkataba wake umevunjwa, kitu ambacho hafahamu na anachohitaji watimize kile walichokubaliana katika majukumu yake.
Kwa sasa Mbeya City ipo chini ya kocha msaidizi Mathias Wandiba, ambaye ataendelea kuwa msimamizi wa timu hiyo.
,
Comments (0)