Posted By Posted On

Azam yavunja rekodi yake msimu 2015/2016

NA HENRY PAUL

TIMU ya Azam katika mchezo wake wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ihefu, imevunja rekodi yake iliyoiweka msimu wa 2015/2016, baada ya kushinda michezo saba mfululizo bila ya kufungwa.

Azam ilivunja rekodi hiyo, baada ya kuifunga Ihefu mabao 2-0, katika mchezo mkali wa ligi hiyo uliochezwa  juzi kwenye Uwanja wa Sokoine, mjini Mbeya.

Msimu wa 2015/2016, Azam ilianza mchezo wake wa kwanza kwa kuifunga Tanzania Prisons mabao 2-1, kisha kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Stand United, kabla ya kuinyuka Mwadui bao 1-0.

Katika mchezo uliofuata, Azam iliibuka na ushindi wa mabao  2-1 dhidi ya Mbeya City na baadaye iliifunga Coastal Union  2-0, kabla ya kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.

Takwimu zinaonesha  Azam imevunja rekodi yake baada ya  juzi kuifunga Ihefu mabao 2-0, ukiwa ni mchezo wa raundi ya saba.

Azam walianza msimu huu kwa ushindi wa  bao 1-0 dhidi ya  Polisi Tanzania, iliifunga Coastal Union mabao 2-0, kabla ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City.

Mchezo uliofuata, Azam ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons bao 1-0, kabla y kuifunga Kagera Sugar mabao 4-2, kisha  kuichapa Mwadui mabao 3-0.

Msimu wa 2015/2016,  kocha wa Azam alikuwa ni Stewart Hall raia wa Uingereza, huku msimu huu  ikiwa chini ya Aristica Cioaba raia wa Romania.

Kwa sasa Azam wanaongoza katika msimamo wa lig hiyo kutokana na pointi 21, baada ya kushinda michezo saba. ikifuatiwa na Simba yenye pointi 13, sawa na Yanga, lakini zikitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *